Tafiti: Miji ya Asia na Marekani inaongoza utoaji Kaboni
15 Novemba 2024Matangazo
Takwimu mpya ambayo inajumuisha uchunguzi na tafiti kuhusu akili mnemba, inaonyesha kuwa miji iliyopo barani Asia na Marekani huchangia pakubwa katika utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira.
Majimbo saba, sita kutoka China yakiongozwa na Shanghai, hutoa zaidi ya tani bilioni 1 ya gesi chafuzi kwa mazingira, huku mji wa Marekani wa Texas ukishikilia nafasi ya sita.
Mataifa yanayoshiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira wa COP29 mjini Baku nchini Azerbaijan, yanajaribu kuweka malengo mapya ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kubaini namna mataifa tajiri yanavyoweza kutoa fedha zaidi ili kuusaidia ulimwengu kufanikisha azma hiyo.