SiasaPakistan
Taliban yakana kushambulia msafara wa ubalozi, Pakistan
23 Septemba 2024Matangazo
Kauli hiyo ya msemaji wa kundi linalofahamika kama "Tehreek-e-Taliban-Pakistan" imetolewa wakati mamlaka za Pakistan zikisema bado zinaendelea na uchunguzi ili kubaini ni nani aliyehusika na shambulio hilo ambalo lilisababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi.
Mabalozi kutoka mataifa Indonesia, Ureno, Kazakhstan, Bosnia, Zimbabwe, Rwanda, Turkmenistan, Vietnam, Iran, Urusi na Tajikistan walishambuliwa hapo jana katika eneo la Malam Jabba wakiwa safarini kwenda Swat Valley, eneo ambalo liliwahi kuwa ngome imara ya kundi la Taliban la Pakistan.
Eneo hilo ni mojawapo ya vituo viwili vya mapumziko nchini Pakistan vinavyopatikana katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa unaopakana na Afghanistan.