Wakati vuguvugu la madai ya katiba mpya likiendelea kufukuta, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoundwa na pande mbili, Zanzibar na Tanganyika, imekiri hii leo bungeni kuwa bado kuna masuala kadhaa ya Muungano ambayo hayajapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na mgawanyo wa mapato unaotokana na hisa za Zanzibar. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu kutoka Dodoma Deo Kaji Makomba.