Tibet na China
27 Machi 2008Wakati rais George Bush wa Marekani mwishoe, ameacha kimya chake jana juu ya mkomoto unaoendeshwa na vikosi vyake vya usalama huko Tibet na juu ya mwito wa kususia michezo ijayo ya Olimpik,China, imezionya nchi za Ulaya kutoatoa ishara zisizofaa kwa Dalai Lama-kiongozi wa waumini wa madhehebu ya Budha wa Tibet.
Isitoshe, polisi nchini Nepal,jirani na Tibet, imewatia nguvuni watibeti 17 kwa kuandamana dhidi ya China mjini Khatmandu.
►◄
Kiasi chai watawa darzeni 2 wa Kitibeti wamefanya maandamano mafupi ya malalamiko mbele ya waandishi habari wa kigeni mjini Lahsa,mji mkuu wa Tibet hii leo.
Watawa hao walipaza sauti kumnyamazisha afisa wa serikali ya China aliekuwa akiwapasha habari waanadishi wa kigeni.Waliituhumu serikali ya china kutoa eleza ukweli juu ya hali hasa inayopita huko Tibet.
Ziara hii ya waandishi habari wa kigeni huko Tibet ni ya kwanza tangu machafuko kuzuka huko mapema mwezi huu.Hapo kabla, rais George Bush wa Marekani alimpigia simu rais Hu Jintao wa China akielezea wasi wasi wake juu ya msukosuko uliozuka Tibet.Rais Bush alimtaka rais Jintao kuanza mazungumzo na Kiongozi wa watibeti aishie uhamishoni Dalai Lama .
Dalai Lama ametuhumiwa na China kuwa nyuma ya machafuko yaliozuka yalioongoza kuuwawa kwa watu kadhaa.Binafsi, Dalai lama amelaani machafuko hayo,lakini amependekeza mazungumzo na watawala wa China.
China ikichukua msimamo mkali na kutooenesha bado kuregeza kamba juu ya swali la Tibet huku sauti zikihanikiza kudai kususiwa michezo ijayo ya Olimpik ya beijing,August mwaka huu,imezionya nchi za umoja wa Ulaya kutotoa ishara zisizo barabara kwa wafuasi wa Dalai Lama.
Mwito wa China umetoka huku mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa kwa mkutano na China -moja ya ajenda likiwa swali la Tibet.Mkutano wao huo unaanza kesho huko Slovenia.Si wazi bado iwapo mawaziri hao wa nje wa ulaya watapima kususia au kutoisusia michezo ya Olimpik ya Beijing.Makamo-waziri mkuu wa Ubelgiji Didier Reynders,hakuondosha uwezekano wa kusisia olimpik endapo hali ya mambo ikichafuka zaidi.
China inadai wafanya-machafuko huko Tibet wamewaua raia 18 wasio na hatia pamoja na polisi 2 wakati viongozi wa Tibet uhamishoni , wametoa idadi ya waliofariki katika mkomoto wa vyombo vya usalama vya China ni kati ya 135 na 140 huku wengine 1,000 wamejeruhiwa na wengine wengi wakiwa kizuizini.
Polisi leo imewatia kizuizini watibeti 17 katika nchi jirani ya Nepal kwa fujo lao katika maandamano dhidi ya china.