Tume ya uchaguzi yathibisha matokeo Georgia
16 Novemba 2024Upinzani unaoungwa mkono na nchi za Magharibi umekosaoa kura hiyo ya Oktoba 26 na kusema ni ya "udanganyifu", huku Umoja wa Ulaya na Marekani zikitaka uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya "ukiukwaji" katika uchaguzi.
Soma pia: Upinzani nchini Georgia waitisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa bunge
Matokeo ya mwisho yaliyotolewa leo Jumamosi ya tume ya uchaguzi yanakipa chama cha Georgian Dream ushindi wa viti 89 katika bunge lenye wabunge 150, ambalo upinzani unataja kuwa ni "haramu" na umekataa kuingia.
Rais Salome Zurabishvili -- akizozana na chama tawala -- pia ameitaja kura hiyo kuwa isiyo halali na kuishutumu Urusi kwa kuingilia kati. Moscow imekanusha madai hayo.
Kiongozi huyo mkuu alijiunga na miito ya upinzani ya kutaka kura mpya, akisema hatatoa amri ya kuitisha bunge jipya.