Ujerumani: Hujuma imefanyaka katika mawasiliano ya baharini
19 Novemba 2024Kauli ya Ujerumani imetolewa chini ya kiwingu cha kuripotiwa na Sweden, uharibifu mwingine wa nyaya za mawasiliano za chini ya bahari. Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius akizungumza pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje mjini Brussels, amesema uharibifu mkubwa umefanywa dhidi ya nyaya za mawasiliano kati ya Finland na Ujerumani na kati ya Sweden na Lithuania na kwamba hatua hiyo ni ishara ya wazi ya kuendelea kwa namna fulani ya hujuma. Pistorius amesema hakuna anayeamini kwamba uharibifu huo umesababishwa na ajali. Jana kampuni ya mawasiliano ya Finland Cinia iliripoti kwamba nyaya za mawasiliano kati ya Helsinki na bandari ya Ujerumani ya Rostock zimekatwa kutokana na sababu zisizojulikana. Na leo maafisa wa Sweden wamesema nyaya za mawasiliano kati ya nchi hiyo na Lithuania nazo hazifanyi kazi.