Ujerumani yafungua Sinagogi jipya Magdeburg
10 Desemba 2023Matangazo
Waziri Mkuu wa jimbo la Sachsen-Anhalt Reiner Haseloff amesema sinagogi hilo jipya linasimamia masuala ya kuishi kwa pamoja kwa amani.
Ameongeza kuwa maisha ya wayahudi katika jimbo hilo yanathaminiwa na kutambuliwa. Kwa upande wake kiongozi wa Baraza la wayahudi Josef Schuster, amesisitiza kuwa leo ni siku ya furaha na ya kujivunia.
Soma zaidi: Scholz asikitishwa na kuenea visa vya chuki kwa Wayahudi
Jengo hilo jipya limegharimu dola milioni 8.1 na lilijengwa kwa hisani ya juhudi za raia wa jimbo hilo waliokusanya michango ya kujenga eneo jipya la kuabudu. Jimbo la Saxony-Anhalt liligharamia sehemu kubwa ya ujenzi wa sinagogi hilo.