Berlin yataka nishati kutokana na upepo Bahari ya Kaskazini
24 Aprili 2023Matangazo
Kulingana na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo, Ujerumani, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi, Denmark, Norway, Uingereza, Ireland na Luxenbourg, zinapania kuongeza nishati hiyo hadi gigawati 300 kufikia 2050.
Mwaka uliopita, kampuni za nishati katika bahari hiyo zilikuwa na uwezo wa kuzalisha takriban gigawati 30.
Hiyo ni kulingana na chama cha kampuni za nishati kutokana na upepo katika kanda hiyo WindEurope, Ujerumani ikichangia gigawatu 8.
De Croo ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo wa kilele, anataka mjadala ujikite kuhusu mbinu za haraka za kujenga mitambo mipya ya kuzalisha nishati itokanayo na upepo ili kuongeza uzalishaji nishati na kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.