Ujerumani yataka Umoja wa Mataifa uishughulikie Yemen
17 Mei 2023Baerbock amesema kuboreshwa kwa uhusiano kati ya nchi za Kiarabu kumeleta matumaini.
Amesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa ndio unaopaswa kuleta amani ya kudumu nchini Yemen.
Baerbock anayefanya ziara ya siku mbili nchini Saudi Arabia ameeleza kwamba matumaini ya kumaliza vita vya Yemen yamejitokeza baada ya Saudi Arabia na Iran kusawazisha uhusiano baina yao.
Waziri huyo wa Ujerumani amesema sasa yapo matumaini makubwa ya kupatikana amani nchini Yemen baada ya vita vya miaka mingi.
Hata hivyo amesisitiza kwamba pande zote zinapaswa kushiriki ili kuweza kufikia lengo la kuleta amani katika nchi hiyo.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani alikutana na mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen na walizungumzia juu ya misaada kwa ajili ya watu wa nchi hiyo.